Neema Ng'asha miaka 15 katika muziki wa injili
- nzalinextlevel
- Apr 1
- 1 min read
Neema Ng'asha,ni Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Tanzania. alianza kuimba tangu akiwa mtoto Sunday school.
Lakini ilipofika mwaka 1998 akiwa kidato cha pili Mungu alimupaka mafuta baada ya kushukiwa na Roho Mtakatifu kwa nguvu sana, tangu hapo akaanza kutunga nyimbo za injili.
Akaanzisha band iliyoitwa Jerusalem band ambayo walikuwa wakiimba na dada yake Martha Ng'asha na vijana wengine pale kanisani.
Mwaka 2010 baada ya kumaliza chuo pale AVU-University of Dar es salaam alingia studio na kurekodi album yake ya kwanza iliyoitwa USINIPITE MWOKOZI.
Mpaka sasa amerekodi album 3 na single nyingi ikiwemo SALAMA aliyoichia Mwezi March 2024.
Mwaka 2024 alifanikiwa kupata tuzo ya Muimbaji bora wa kike kutoka kampuni ya Eagle's Entertainment

Comentarios